Alhamisi 19 Februari 2026 - 17:24
Je! Ukisahau nia ya kufunga, funga yako itakuwa sahihi?

Hawza/ Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amejibu istifta (swali la kisheria) kuhusiana na mwenye “kusahau nia ya kufunga.”

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Khamenei ametoa jibu kwa istifta hiyo kuhusu “kusahau nia ya kufunga,” ambalo linawasilishwa kwenj kama ifuatavyo:

Kusahau nia ya kufunga

Swali:
Ikiwa mtu alikuwa tayari na uamuzi wa hakika tangu awali wa kufunga siku maalumu — kama siku ya Dahwal-Ardh — lakini akasahau, na siku hiyo akala chakula au akanywa maji, kisha akakumbuka, je! Hukumu ya funga yake ya siku hiyo ni ipi?

Jibu:
Ikiwa alikuwa ameweka nia ya kufunga tangu usiku uliotangulia kwa ajili ya kesho, funga yake ni sahihi. Lakini kama alikuwa amesahau na hakuweka nia, na alikuwa tu na azma ya jumla ya kufunga tangu siku zilizopita, hilo halitoshi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha